Maji ya chumvi kufanyiwa utafiti wa tiba ya corona.


Majaribio ya utumiaji wa maji ya chumvi kama tiba ya virusi vya corona yatafanyika na watafiti huko Edinburgh.


Utafiti wa awali ulionesha kwamba dawa za kutengenezwa nyumbani zinaweza kusaidia kupuguza makali ya dalili za virusi vya corona kama ilivyo kwa homa.

Utafiti huo ulionesha kwamba watu wanaosukutua na kusafisha pua zao kwa maji ya chumvi kikohozi kinapugua, kubana kwa mbavu kunapungua huku wagonjwa wakionekana kupona kwa haraka.

Wanasayansi wa chuo Kikuu cha Edinburgh watachunguza ikiwa dawa hiyo pia inaweza kusaidia watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona.

Utafiti huo kwa sasa hivi unasajili watu wenye dalili za ugonjwa wa Covid-19 ambao wamethibitishwa kupata maambukizi.

Utafiti wa awali ulisajili watu wazima ambao wamebainishwa kuwa na maambukizi katika mfumo wa juu wa upumuaji kwa siku mbili kulikochukuliwa kama homa.

Waligawanywa kwenye makundi mawili huku kundi la kwanza likitakiwa kusukutua na kusafisha njia ya pua kwa maji ya chumvi wakati wanahisi kufanya hivyo.

Kundi jingine likawa linatibu homa hiyo kwa njia ya kawaida.

Washiriki wote waliweka kumbukumbu ya dalili zao kwa wiki mbili. Pia walipimwa kuangaliwa kiwango cha virusi hivyo vya homa ndani ya pua zao.

Watafiti hao wanasema waliokuwa wakisafisha njia ya pua na kusukutua kwa maji ya chumvi, homa yao ilikuwa ya muda mfupi, na kupunguza uwezekano wa kusambaa hadi kwa familia zao, wakapona haraka huku wakiwa na uwezekano wa chini wa kutumia dawa zinazouzwa kwa maduka ya dawa.

Profesa Aziz Sheikh, mkurugenzi wa chuo kikuu cha Usher, amesema: "Sasa hivi tunaingia kwenye ya utumiaji wa maji ya chumvi kwa waliothibitishwa kupata maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19, na ni matumaini yetu kwamba yataonesha matokeo chanya ya kupunguza athari za usambaaji wa maambukizi.

"Kinachohitajika ni chumvi, maji na kuelewa mchakato wa jinsi mchanganyiko huo unavyotengenezwa. Unastahili kufanya kazi, ikiwa utaonesha ufanisi, itakuwa njia rahisi, isio na gharama na yenye kutekelezeka sehemu yoyote ile."

Utafiti huo umefadhiliwa na Breathe - kituo cha utafiti wa afya ya njia ya upumuaji.


Comments

Popular posts from this blog

VITALI MAEMBE KUWANIA UBUNGE BAGAMOYO

MWANAMUZIKI MAARUFU AACHA MUZIKI KWA MSONGO WA MAWAZO