MWANAMUZIKI MAARUFU AACHA MUZIKI KWA MSONGO WA MAWAZO




Vanessa mdee ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa kike nchini Tanzania na barani Afrika.

Siku kadhaa zilizopita Mdee alitangaza kuacha shughuli zote za muziki na burudani kupitia Podcast yake inayoitwa 'Deep dive with Vanessa Mdee'

Katika maelezo yake anasema amekua akikabiliana na msongo wa mawazo
Vanessa ameongezea pia gharama za kuendesha shughuli ya muziki zilikua kubwa kuliko faida yake.

''Nafanya show kwa dola 1000 , hapo unatakiwa kutoa gharama ya kila kitu, kuwalipa watu, mimi mwenyewe, sehemu ya kuishi, gharama za kusafiri, hapo hapo ule, ujenge, usaidie familia''.

Vanessa Amefikia uamuzi huu baada ya kuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 10.

Anasema kila mwaka amekua akirudia mfumo wa Maisha huo huo, amekua akiridhisha wengine lakini hakua na furaha yeye binafsi.

''Nimekua nikiridhisha watu wengine kila siku kwa miaka 13, nimekua kwenye muziki kwa miaka saba, lakini nimeanza kujihusiha zaidi ya miaka 13, na kila siku hali ni ile ile''.

Baada ya kutoa maamuzi yake Vanessa anasema amepata ujumbe wa wasanii mbalimbali wakimwambia amefanya uamuazi mzuri, na baadhi wanapitia hali kama yake lakini hawajapata ujasiri wa kuweka wazi.

''Baada ya kuongea kwenye podcast yangu, nilipokea ujumbe kutoka kwa watu, wengine wanamuziki, wananiambia asante sana, mimi napitia asilimia 100 hali kama yako, maamuzi yangu hayakua mepesi na ni ngumu kwa mtu ambaye hayupo kwenye tasnia sio rahisi kuelewa"alisema Vanessa.


Comments

Popular posts from this blog

VITALI MAEMBE KUWANIA UBUNGE BAGAMOYO