Posts

TRADITIONAL MUSIC IN TANZANIA.

Image
  Young talented musician from Africa Afrovalentine want to prove that African traditional music is alive.           Afrovalentine (Valentine Mbassa) inherited natural talent from his great grandfather Mbassa Muhumba Mtelegani who was one of the respected and well known traditional Ngoma players as well as traditional music singers in 1910 and years after. This took place in Ukerewe Island, a region of Mwanza.         When Valentine entered primary school at the age of 7 he started music in Sunday schools as a percussionist and singer. The inspiration from his great grandfathers music talent gave him a natural and free feel for music, especially traditional. After graduating secondary level, he decided to join with Zawose Spirit Band, a group from the legacy of Dr. Hukwe Ubi Zawose, led by Sinaubi Zawose and his father Lukas Ubi Zawose in 2018.        Valentine was playing traditional Ngoma and singing prior to that time, though presently he is in Zawose Spirit Band but does his own pr...

Maji ya chumvi kufanyiwa utafiti wa tiba ya corona.

Image
Majaribio ya utumiaji wa maji ya chumvi kama tiba ya virusi vya corona yatafanyika na watafiti huko Edinburgh. Utafiti wa awali ulionesha kwamba dawa za kutengenezwa nyumbani zinaweza kusaidia kupuguza makali ya dalili za virusi vya corona kama ilivyo kwa homa. Utafiti huo ulionesha kwamba watu wanaosukutua na kusafisha pua zao kwa maji ya chumvi kikohozi kinapugua, kubana kwa mbavu kunapungua huku wagonjwa wakionekana kupona kwa haraka. Wanasayansi wa chuo Kikuu cha Edinburgh watachunguza ikiwa dawa hiyo pia inaweza kusaidia watu waliopata maambukizi ya virusi vya corona. Utafiti huo kwa sasa hivi unasajili watu wenye dalili za ugonjwa wa Covid-19 ambao wamethibitishwa kupata maambukizi. Utafiti wa awali ulisajili watu wazima ambao wamebainishwa kuwa na maambukizi katika mfumo wa juu wa upumuaji kwa siku mbili kulikochukuliwa kama homa. Waligawanywa kwenye makundi mawili huku kundi la kwanza likitakiwa kusukutua na kusafisha njia ya pua kwa maji ya chumvi wakati wanahisi kufanya hivyo...

MWANAMUZIKI MAARUFU AACHA MUZIKI KWA MSONGO WA MAWAZO

Image
Vanessa mdee ni miongoni mwa wanamuziki maarufu wa kike nchini Tanzania na barani Afrika. Siku kadhaa zilizopita Mdee alitangaza kuacha shughuli zote za muziki na burudani kupitia Podcast yake inayoitwa 'Deep dive with Vanessa Mdee' Katika maelezo yake anasema amekua akikabiliana na msongo wa mawazo Vanessa ameongezea pia gharama za kuendesha shughuli ya muziki zilikua kubwa kuliko faida yake. ''Nafanya show kwa dola 1000 , hapo unatakiwa kutoa gharama ya kila kitu, kuwalipa watu, mimi mwenyewe, sehemu ya kuishi, gharama za kusafiri, hapo hapo ule, ujenge, usaidie familia''. Vanessa Amefikia uamuzi huu baada ya kuwa katika tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 10. Anasema kila mwaka amekua akirudia mfumo wa Maisha huo huo, amekua akiridhisha wengine lakini hakua na furaha yeye binafsi. ''Nimekua nikiridhisha watu wengine kila siku kwa miaka 13, nimekua kwenye muziki kwa miaka saba, lakini nimeanza kujihusiha zaidi ya miaka 13, na kila siku hali ni ile il...

VITALI MAEMBE KUWANIA UBUNGE BAGAMOYO

Image
 Hatimaye Mwanamuziki Nguli anayefanya muziki wa Asili Maembe Vitali "Mswahili" Leo amefunguka rasmi kwa umma kuwa ameamua kujitosa kuomba kujiunga na chama chochote cha siasa ili kiweze kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Wilaya ya Bagamoyo.  Kupitia mitandao ya kijamii Maembe amesema kuwa, yeye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, na kwa kuwa sheria za nchi yetu aziruhusu mtu yeyote kugombea bila kupitia chama chochote (Mgombea binafsi), ameamua kuweka wazi Itikadi zake ili kama kipo chama kitakachozikubali basi kiweze kumkaribisha na kumpa ridhaa hiyo.  Maembe ameeleza kuwa yeye ni mjamaa na anaamini kuwa binadamu wote ni sawa na yupo kinyume na ubaguzi wowote wa rangi, dini, Kabila na vilevile yupo kinyume na ubaguzi wa Aina yeyote unaodunisha Utu wa mtu, na kusisitiza kuwa "hawezi kubadilika kwenye hilo".  Pia mkali huyo wa vibao "Sumu ya Teja", "vuma ","kudu" na nyinginezo, ameeleza pia yeye ni Mwanamuziki wa um...